Psalms 13

Sala Ya Kuomba Msaada

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1 a bMpaka lini, Ee Bwana? Je, utanisahau milele?
Utanificha uso wako mpaka lini?
2 cNitapambana na mawazo yangu mpaka lini,
na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu?
Adui zangu watanishinda mpaka lini?

3 dNitazame, unijibu, Ee Bwana Mungu wangu.
Yatie nuru macho yangu,
ama sivyo nitalala usingizi wa mauti.
4 eAdui yangu atasema, “Nimemshinda,”
nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka.

5 fLakini ninategemea upendo wako usiokoma;
moyo wangu unashangilia katika wokovu wako.
6 gNitamwimbia Bwana,
kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.
Copyright information for SwhNEN